Ampiga Mtu Risasi Kisa Ubishani wa Mziki.

Ampiga Mtu Risasi Kisa Ubishani wa Mziki.

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa majina ya Cesar Esquivel Estrada, mwenye umri wa miaka 46 alimfyatulia Risasi na kumuua Mwanaume mwingine aliyefahamika kama Socorro Camacho mwenye umri wa miaka 54 aliye kejeli Wimbo uliochezwa kwenye Jukebox na Estrada katika Mgahawa wa Kimeksiko unaojulikana kama Fort Lauderdale uliopo Florida, huko Marekani.

Inasemekana katika Tukio hili la kusikitisha lilitokea Jumatatu jioni, Septemba 24, 2024, lilianza kama majibizano ya maneno kati ya Wanaume hao wawili, ambapo Estrada alidaiwa baadae kumpiga risasi Camacho baada ya mzozo kufikia pabaya.

Kulingana na Shahidi katika eneo la tukio alisema, Estrada alicheza wimbo ambao Mwathirika hakuupenda na akamwambia Estrada kwa kufoka “wewe sio Mexico halisi ikiwa unacheza muziki huo.”

Shahidi alisema, Mwathiriwa ambaye alitusi wimbo uliochezvwa na Estrada, alichomoa silaha yake nje na kufyatua raundi ya kwanza, kisha Estrada alidaiwa Kujibu na hatimaye kumuua.

Inaripotiwa kuwa, baadae Mwanaume huyo alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya daraja la kwanza, huku Rekodi zikionyesha kuwa Estrada alikuwa Nchini Marekani kinyume cha sheria, kwani alikuwa na zuio la uhamiaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button