Meya Wa New York Asomewa Mashtaka ya Ufisadi.

Meya Wa New York Asomewa Mashtaka ya Ufisadi.

Meya wa jiji la New York Eric Adams, amepandishwa kizimbani kwa mashtaka matano yanayohusiana na ufisadi, udanganyifu, na kujihusisha na michango ya kampeni kutoka kwa raia wa kigeni.

Hayo ni kwa mujibu wa hati ya mashtaka yenye kurasa 57 iliyotangazwa Alhamisi asubuhi.

Mashtaka yanaeleza kuhusu vitendo vya uhalifu vilivyodaiwa kuanzia mwaka 2014, wakati Adams akiwa kiongozi wa eneo la Brooklyn.

Kwenye hati hiyo, inadaiwa kwamba Adams alikubali faida zisizo za kisheria, kama vile safari za kifahari za kimataifa kutoka kwa wafanyabiashara matajiri wa kigeni na mmoja akitajwa kutokea serikali ya Uturuki.

Adams anatarajiwa kufanya kikao chake cha kwanza mahakamani ljumaa. Aliutangazia umma kuwa hakuwa na mshangao kuhusu mashtaka hayo na alihimiza watu kusubiri utetezi wake kabla ya kutoa maamuzi.

Wakili wake alimtetea Adams, akisisitiza kuwa meya alishauriana na wafanyakazi wake kutokukubali fedha za kigeni.

Mashtaka hayo yanatishia taaluma ya ya kisiasa ya Eric Adams, huku wanasiasa maarufu wa New York wakitaka ajiuzulu.

Gavana wa New York, Kathy Hochul, alisema kuwa Adams anapaswa kutumia siku chache kufikiria hali hiyo na kutafuta njia bora ya kuendelea.

Adams amekuwa akitumikia kama meya tangu Januari 2022, akijitambulisha kama uso mpya wa Chama cha Democrat, lakini amekabiliwa na changamoto kadhaa za jiji, ikiwa ni pamoja na mgogoro wa wahamiaji na usalama wa huduma za usafiri Wa umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button