P Diddy Hana Wasiwasi Kuuliwa Gerezani

P Diddy Hana Wasiwasi Kuuliwa Gerezani.

P Diddy msanii maarufu wa muziki na mfanyabiashara, anaripotiwa kutokuwa na wasiwasi kuhusu kuwekewa sumu kwenye chakula chake gerezani kama ambavyo wengine wanahifia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TMZ, uvumi kwamba Diddy ameacha kula kwa sababu ya hofu ya kupewa sumu si kweli.

Chanzo kilicho karibu naye kinasema kwamba anaendelea kula chakula cha kawaida cha gerezani kama wafungwa wengine.

Diddy yupo kwenye jela ya Metropolitan (MDC) huko Brooklyn, baada ya kukataliwa dhamana mara mbili, hata baada ya timu yake ya mawakili kutoa ofa ya kifurushi cha dola milioni 50 (takribani shilingi bilioni 125 za Tanzania) ili aweze kuhudhuria kesi yake akiwa uraiani.

Anakabiliwa na mashtaka ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya biashara ya ngono, njama ya uhalifu, na usafirishaji wa watu kwa ajili ya ukahaba.

Ingawa anahifadhiwa kwenye kitengo maalum mbali na wafungwa wa kawaida, na kuwekwa chini ya uangalizi wa kuzuia kujiua, timu yake ya sheria inasema hana mawazoya kujiua.

Hata hivyo, Suge Knight, adui wa zamani wa Diddy, amemtahadharisha kuwa afahamu hatari zinazomkabili kutoka kwa wafungwa wengine.

Lakini sumu kwenye chakula haimo kwenye orodha ya wasiwasi wa Diddy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button