Baraza La Sanaa Basata Tanzania Lamteua #MrishoMpoto Kuwa Balozi na Msemaji wa Basata.

Nyota ya Msanii nguli na mkongwe kwenye Sanaa Mrisho Mpoto (mjomba) nyota yake inazidi kung”a kwa mara nyingine.

Baada ya kupata teuzi mbalimbali za wizara na Serikali leo leo Ameteuliwa tena kuwa BALOZI na na Msemaji wa Baraza la sanaa BASATA Afla hiyo imefanyika katika Ofisi za Basata Jijini Dar es salaam

Katibu Mtendaji wa Baraza Dr Mapana amefanya utambulisho wa mabalozi hao wawili akiwembo Mkurugenzi wa na Mwanzilishi wa Bongo Star Sarch Madamu Rita leo tarehe 15/8/2023

Mrisho Mpoto amepokea kwa furaha kubwa uteuzi huo na kusema sasa wakati umefika wasanii walioko pembezoni kupata jukwaa la kuonyesa kazi zao, Mpoto amesisitiza kuimarisha Maadili na uadilifu na kutoa Elimu kwa wasanii wenzake Kuheshimu sheria za Nchi xna kufanya kazi zenye maadili na zenye maslahi mapana kwa Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button