Congo – Rais Félix Tshisekedi amamchagua Judith Suminwa Tuluka kuwa Waziri Mkuu, uteuzi huo unamfanya Judith kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo
Rais Félix Tshisekedi amamchagua Judith Suminwa Tuluka kuwa Waziri Mkuu, uteuzi huo unamfanya Judith kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika taifa hilo ambalo linakabiliwa na changamoto chungumzima ikiwemo masuala ya usalama upande wa mashariki.
Suminwa anachukua nafasi ya Jean-Michel Sama Lukonde aliyeongoza serikali tangu Februari 2021 kabla kujiuzulu Februari 21, mwezi mmoja baada ya kuapishwa kwa Rais Tshisekedi kwa muhula wa pili na wa mwisho.







