DKT. BITEKO AWATAKA WATANZANIA KUTOGAWANYIKA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU
✅️ Asema Serikali ya Rais Samia itahakikisha miradi ya maendeleo inagusa wananchi
✅️Aelezea upekee wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
✅️Asema Rais Samia anasema na kutenda
Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi kutogawanywa kwa itikadi ya dini wala siasa wakati huu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Ubunge na Udiwani kwa manufaa ya Taifa.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Aprili 23, 2025 wilayani Monduli mkoani Arusha wakati akizungumza na wanannchi mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Esilalei.
“ Ninatamani kuona hatugawanyiki na mtu yoyote wala hatuwekwi kwenye makundi ya dini wala ukabila. Nataka niwaombe wananchi wa Monduli pendaneni na shirikianeni na uchaguzi utakapofika chaguaneni kwa haki,” amesema Dkt. Biteko.
Amewataka wananchi wa Monduli kuutunza mradi huo wa maji wa Esilalei “ Nawapongeza Wizara ya Maji na RUWASA kwa kusimamia mradi huu mzuri na wa uhakika, bila shaka mtaona itakapofika Desemba mwaka huu awamu ya pili ya mradi itakuwa imekamilika,”
Pia, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inawapenda wananchi wa Monduli na inawapongeza kwa uchapakazi wao kwenye kilimo na ufugaji.
Aidha, amewataka wachape kazi na kuwa Rais Samia amefikisha mradi huo wa maji kwa kuwa anapenda pia mifugo yao istawi.vilevile, amesema kuwa Rais Samia amemtuma kuwahakikishia wananchi hao kuwa wafugaji nchini wanakuwa daraja la juu kama walivyo wananchi wengine.
Aidha, amesema wananchi hao wanachohitaji ni Serikali tu iwapatie nyenzo kama maji, umeme na barabara ili kufanikisha shughuli zao ambapo tayari Rais Samia ameapa kuwapatia nyenzo hizo.
Kuhusu umeme, Dkt. Biteko amesema kuwa vijiji vyote vya Wilaya ya Monduli vimepata umeme na katika vitongoji 236, vitongoji 72 vimepata umeme na vilivyosalia vitapata huduma hiyo mara baada ya Uchaguzi Mkuu.
Akijibu ombi la Mbunge wa Monduli, Mhe. Freddy Lowasa “ Nguzo za umeme 20 alizoomba Mhe. Mbunge kuanzia Alhamisi hadi wiki inayokuja tutaanza kuona watu wa hapa wanapata umeme bila masharti yoyote