Donald Trump na Mpango wa Kuiokoa Tiktok Marekani
Donald Trump na Mpango wa Kuiokoa Tiktok Marekani
Rais mteule wa Marekani DonaldTrump anafikiria kutoa amri ya kiutendaji ambayo inaweza kuchelewesha marufuku ya TikTok nchini Marekani, na hivyo kutoa muda zaidi wa kujadili uwezekano wa kuiuza kwa mnunuzi wa Marekani.
Programu hiyo, ambayo ina watumiaji milioni 170 nchini Marekani, inakabiliwa na marufuku ifikapo Januari 20 isipokuwa iuzwe kwa kampuni ya Marekani.
Trump, ambaye hapo awali aliunga mkono marufukunhiyo, ameonyesha nia ya kuiokoa TikTok Marekani.
Hata hivyo, hakuna maendeleo dhahiri kuhusu mauzo hayo, huku ByteDance, mmiliki wa Kichina wa TikTok, akipinga wazo hilo.
Baadhi ya wabunge wamemhimiza Rais Biden kuchelewesha marufuku hiyo, lakini haijulikani kama ataingilia kati.