Gavana Ashtakiwa Kutumia Pesa Kuimarisha Usalama Wake.
Gavana Ashtakiwa Kutumia Pesa Kuimarisha Usalama Wake.
Baada ya tukio la nyumba yake kushambuliwa kwa mabomu ya moto mapema mwaka huu, Gavana wa Pennsylvania JoshShapiro anakabiliwa na uchunguzi mpya kuhusu matumizi ya fedha za umma kwa ajili ya ulinzi wa makazi yake binafsi.
Kamati ya wabunge wa Republican (GOP) imepitisha uamuzi wa kutoa samanzi tatu ili kupata rekodi zinazohusiana na matumizi ya takribani dola milioni 1 zilizotumika kuboresha ulinzi wa nyumba yake ya binafsi kwenye viunga vya Philadelphia.
Kamati hiyo inataka:
Hati za usanifu na zabuni za maboresho ya ulinzi katika makazi yake ya binafsi.
Kumbukumbu za mawasiliano kati ya serikali ya jimbo na Halmashauri ya eneo la makazi ya Shapiro.
Taarifa za safari za ndege binafsi zilizofanywa na Ofisi ya Gavana katikati ya Januari, zikiwemo orodha za abiria na stakabadhi za malipo.
Samanzi hizo zimeelekezwa kwa:
1. Polisi wa Jimbo la Pennsylvania,
2. Afisa wa rekodi za wazi wa mji anakoishi Shapiro,
3. Kampuni ya ndege binafsi iliyopewa kazi ya kusafirisha ofisi ya gavana.
Wote wametakiwa kutoa majibu na nyaraka hizo kabla ya Januari 16, 2026.
Wakosoaji wa uchunguzi huu wanasema kamati hiyo inatumia tukio la mashambulizi kama sababu ya kisiasa, huku wanaounga mkono wakisisitiza kuwa matumizi ya fedha za umma katika mali binafsi lazima yawekwe wazi ili kuepuka matumizi mabaya na kuweka mfano sahihi kwa magavana wa baadaye.





