Israel yatangaza kuuawa kwa kamanda wa kijeshi wa Hamas
Israel yatangaza kuuawa kwa kamanda wa kijeshi wa Hamas
Jeshi la Israel limetangaza kuwaua wanachama watano wa Hamas, akiwemo kamanda wa kijeshi, katika operesheni iliyofanyika Jumatatu Septemba 14, 2026 huko Gaza. Gazeti la The Times of Israel limeripoti kuwa jeshi la Israel limetangaza kuwa vikosi vyake na shirika la usalama wa ndani la lIsrael, Shin Bet, vimeongeza kasi ya operesheni zao za kupambana na ugaidi katika Ukanda wa Gaza wiki za hivi karibuni.
Vyanzo vya habari vya Hamas pia vimethibitisha kifo cha kamanda wa kijeshi wa Hamas ambaye gari lake limeripotiwa kulengwa na Israel ni Ahmad al-Batsh, anayejulikana kwa jina la utani ‘Abu Osama’. Shirika la Habari la Fars – ambalo lina uhusiano wa karibu na Walinzi wa Mapinduzi – liliandika usiku wa Jumatatu, likinukuu ‘Gaza Al-Aan’, kwamba alikuwa Kamanda wa Vikosi vya lzz al-Din al-Qassam na aliuawa kufuatia shambulio la anga la lsrael.
Pia Al Jazeera imeandika kuhusu namna ambavyo mwanachama huyo mwandamizi wa Hamas aliuawa, ikieleza kuwa aliuawa katika shambulio la anga dhidi ya gari katika Mtaa wa Al-Saftawi, ulioko kaskazini mwa Jiji la Gaza (magharibi mwa Jabalia).





