Sita wafariki dunia ajali ya meli Indonesia, 129 hawajulikani walipo

Sita wafariki dunia ajali ya meli Indonesia, 129 hawajulikani walipo

Watu 129 hawajulikani walipo nchini Indonesia baada ya meli ya abiria ya Virgo Transport 8 kupinduka katika Bahari ya Java, huku watu sita wakithibitishwa kufariki na 108 kuokolewa.

Kwa mujibu wa Reuters, ajali hiyo ilitokea Jumapili, Septemba 13, 2026, wakati meli hiyo ikiwa safarini kutoka Surabaya, Mashariki mwa Java, kuelekea Banjarmasin, Kusini mwa Kalimantan. Meli hiyo ilikuwa imebeba watu 243, wakiwemo abiria 213 na wafanyakazi 30.

Reuters imeripoti kuwa meli hiyo ilipoteza mavwasiliano na mamlaka karibu saa 2:00 asubuhi kwa saa za Indonesia baada ya kukumbwa na hali mbaya ya hewa baharini.

Baadaye iliripotiwa kuwa meli hiyo ilipinduka katika eneo la Masalembo, takribani kilomita 148 kutoka Banjarmasin. Mkuu wa Wakala wa Kitaifa wa Utafutaji na Uokoaji wa Indonesia (Basarnas), Mohammad Syafii, amesema shughuli za uokoaji zimeongezwa, huku waokoaji wakitumia meli, ndege na vikosi maalumu vya uokoaji chini ya maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button