Israeli na Gaza Wafikia Makubaliano ya Kumaliza Vita.
Israeli na Gaza Wafikia Makubaliano ya Kumaliza Vita.
Israel na Hamas wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kumaliza vita vilivyodumu miezi 15 huko Gaza, kulingana na chanzo kilichofahamishwa kuhusu mazungumzo hayo, kama ilivyoripotiwa na BBC.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya miezi ya mazungumzo, ambapo Qatar ilikuwa mmoja wa wapatanishi wakuu.
Hamas ilishambulia kusini mwa lsraeli mnamo tarehe 7 Oktoba 2023, na kuua takriban watu 1,200 na kuwachukua mateka 251 kwenda Gaza.
Shambulio hilo lilisababisha mashambulizi makubwa ya kijeshi ya Israeli dhidi ya Gaza, ambap0 zaidi ya Wapalestina 46,000 wameuawa, kulingana na wizara ya afya inayoongozwa na Hamas.