Jaji Chande: Mbinu 16 zilitumika kufanya vurugu

Jaji Chande: Mbinu 16 zilitumika kufanya vurugu

Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Mohamed Chande, amesema uchunguzi umebaini kuwepo kwa mbinu 16 zilizotumiwa na wahusika wakuu na waratibu wa ghasia zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi huo.

Amesema baadhi ya mbinu hizo ni pamoja na kuweka vizuizi barabarani, kuchoma moto, matumizi ya pikipiki, pamoja na alama za kutambuana kati ya wahusika.

“Matukio haya yalikuwa na malengo ya kuzuia na kuvuruga uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025. Hii inadhihirishwa na uharibifu wa vituo vya kupigia kura, kufikisha ujumbe kwa Serikali, na baadhi ya matukio ya uporaji na wizi; pili, vijana kufikisha ujumbe kwa Serikali ili iwasikilize changamoto zao,” amesema.

Jaji Chande amesema hayo leo, Alhamisi, Aprili 23, 2026, Ikulu, jijini Dar es Salaam kabla ya kukabidhi ripoti ya tume hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button