Jaji Chande: Ripoti imebeba Taifa kutibu majeraha na kuwajibika

Jaji Chande: Ripoti imebeba Taifa kutibu majeraha na kuwajibika

Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Mohamed Chande Othman amesema ripoti ya tume hiyo inalenga kusaidia Taifa kutibu majeraha, kuwajibika na kujifunza ili kusonga mbele.

“Tunaamini ripoti hii na mapendekezo yake yatabeba dhamira ya taifa ya kutibu majeraha, kuwajibika pale panapostahili na muhimu zaidi kujifunza na kusonga mbele,” amesema.

Jaji Chande ameyasema hayo leo Alhamisi, Aprili 23, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha akipokea Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button