Kesi Uchaguzi Serikali za Mitaa,Serikali yapewa 14 Kutoa Majibu

Kesi Uchaguzi Serikali za Mitaa,Serikali Yapewa Siku 14 Kutoa Majibu

Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imeipa Serikali ya Tanzania siku 14 kuwasilisha majibu na kiapo kinzani katika shauri la kupinga Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Novemba 27, 2024 na Agosti 15, mwaka huu mchakato wa uchaguzi huo utaanza.

Lakini wanaharakati watatu wanaojitambulisha ni raia wa Tanzania waliosajiliwa katika Daftari la Kudumu la
Wapigakura, wamefungua shauri la kuupinga kwa utaratibu wa mapitio ya Mahakama.

Shauri hilo limefunguliwa na Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Bob Wangwe, mwanahabari mstaafu, Ananilea Nkya na Bubelwa Kaiza na wajibu maombi ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika shauri hilo linalosikilizwa na Jaji David Ngunyale, wanaharakati hao wanapinga kanuni za uchaguzi huo za mwaka 2024 zilizotungwa na Waziri wa Tamisemi,
wakihoji mamlaka yake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button