KIUNGO HATARI WA ULINZI WA MANYEMA ANANUKIA AZAM FC

🎙️Klabu ya Azam FC imedhamiria kufanya Makubwa msimu ujao ikiwa mpaka sasa inaelezwa imepeleka Ofa kwa Kiungo mkabaji Charve Onoya wa Manyema ya Congo ambaye anatajwa kua na nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi kuu ya nchini humo.

Mpaka sasa Kiungo huyo ambaye ameshinda tuzo za Mchezaji bora wa Mwezi mara 2 ameshafunga bao 5 na Assist 7 huku akiisaidia Manyema kua nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Pia kiungo huyu mwenye miaka 21 ni nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo Chini ya miaka 23 na anacheza kikosi Cha CHAN.

Mbali na taarifa hizo klabu za TP Mazembe, AS Vita na FC Lupopo zote za Congo zinatajwa kuwania saini yake lakini mwenyewe ameonesha nia ya kutoka Nje ya Congo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button