Kuwait Yadungua Ndege 3 Zakivita za Marekani Kwa Bahati Mbaya.
Kuwait Yadungua Ndege 3 Zakivita za Marekani Kwa Bahati Mbaya
Ndege tatu za kivita za Marekani zimeanguka nchini Kuwait siku ya jana Jumatatu kutokana na “tukio la kirafiki la kudunguliwa,” jeshi la Marekani lilisema katika taarifa. Walinzi wa anga wa Kuwait walizidungua kwa bahati mbaya ndege za kivita za F-15E Strike Eagle siku ya kuamkia jana jumatatu. Marubani wote sita walitolewa salama baada ya shambulizi hilo, Kamanda Mkuu wa Marekani alisema.
Chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa, kwa mujibu wa CENTCOM. Ndege hizo zilikuwa zikiruka kuunga mkono operesheni ya kijeshi dhidi ya Iran, iliyopewa jina la Operesheni Epic Fury.
Wizara ya ulinzi ya Kuwait ilikuwa imesema mapema Jumatatu asubuhi kwamba ndege “kadhaa” za kivita za Marekani zilianguka lakini haikubainisha ni ngapi hasa au ni nini kilisababisha. Ndege za kivita kila moja anagharimu makumi ya mamilioni ya dola.
Kauli hiyo inakuja baada ya video zilizowekwa eneo la CNN kuonyesha ndege ya kivita ikianguka Kuwait na rubani wake akichukua hatua salama na kujifyatua ndani ya ndege na kushuka kwa parachuti.





