Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 7 Februari 2024 saa 6:01 usiku. Kwa mwezi Februari 2024, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.
Dar es Salaam Petroli itauzwa Tsh. 3,051, Dizeli Tsh. 3,029 na Mafuta ya Taa Tsh. 2,840 kwa Lita 1. Tanga Petroli itauzwa Tsh. 3,064, Dizeli Tsh. 3,196, Mafuta ya Taa Tsh. 2,886. Mtwara Petroli Tsh. 3,112, Dizeli Tsh. 3,354 na Mafuta ya Taa Tsh. 2,913 kwa Lita Moja ikiwa ni bie za Rejareja.
EWURA imesema kupungua kwa Bei za Mafuta kunatokana na kushuka kwa Bei za bidhaa hizo katika Soko la Dunia kwa wastani wa 10.66% kwa Petroll, 11.20% kwa Dizeli, 5.82 kwa Mafuta ya Taa pamoja na kupungua bei za uagizaji Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.





