Manara sababu hizi Zilinipelekea Kuondoka Simba
Manara Sababu hizi Zilinipelekea Kuondoka Simba.
Leo, kwenye mahojiano na kipindi cha
Powerbreakfast cha @CloudsFMtz, aliyekuwa msemaji wa @simbasctanzania, Haji Manara, ameweka wazi sababu ya kuondoka kwake kwenye klabu hiyo.
Akihojiwa, Manara alikanusha madai kwamba aliondoka kwa sababu ya Mwenyekiti wa Simba, Mohammed Dewji (Mo) au aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbra Gonzalez.
“Mimi Simba sikuondoka kama wengi wanavyodhani sababu ni ya Mo. Mimi Simba nimeondoka kwa sababu ya msingi wala sio Barbra kama watu wengi wanavyodhani.Mimi alienifanya niondoke Simba ni Salim Try Again,” alisema Manara.
Aliendelea kufafanua kuwa mazingira yalikuwa magumu kwake kufanya kazi chini ya ushawishi wa Try Again, ambaye alikuwa na nguvu kubwa ndani ya klabu.
“Yaani alinitengenezea mazingira magumu mimi kufanya.. very very powerful (Try Again). Yaani Simba ni yeye, yeye ni Simba kuliko mtu yeyote kwa kipindi kile.
Alikuwa na nguvu kubwa katika ushawishi kwa maana ya Mohammed na Barbra, aliongeza @hajismanara Kauli hizi zinalenga zaidi uhusiano wa viongozi ndani ya klabu na jinsi maamuzi yanavyofanyika.