Marekani Yaamua Tiktok Ifungwe au iuzwe
Marekani Yaamua Tiktok Ifungwe au iuzwe
Mahakama ya Rufaa ya D.C. imetangaza uamuzi wa kuunga mkono sheria inayotaka ByteDance, kampuni mama ya TikTok kutoka China, kuuza hisa zake za programu hiyo ifikapo Januari 19, 2025, la sivyo itakabiliwa na marufuku kote Marekani.
Sheria hiyo, inayojulikana kama Protecting Americans from Foreign Adversary Controlled Applications Act, imeelezvwa kuwa imelenga moja kwa moja kulinda usalama wa taifa.
Hata hivyo, TikTok imepinga hatua hiyo, ikidai inakiuka haki ya Kifungu cha Kwanza cha Katiba ya Marekani (First Amendment).
Mahakama, kwa upande wake, imesisitiza kuwa ushahidi wa serikali ya Marekani kuhusu hatari za kiusalama una uzito mkubwa, ikizingatia ushawishi wa programu hiyo duniani na uwezekano wa matumizi mabaya.