Roma Anzisha Kampeni Kumuunga Mkono Nay Wamitego kwa Kusimama na Watanzania.

Roma Anzisha Kampeni Kumuumga Mkono Nay Wamitego Kusimama na Watanzania.

Baada ya @naytrueboytz kutoa wimbo
wake mpya “Nitasema”, ambao unagusa changamoto za kijamii na kupaza sauti za raia wa kawaida, kampeni ya kumuunga mkono imeanzishwa na msanii mwenzake
Roma. @roma_zimbabwe, kupitia mitandao ya kijami, aliwahamasisha mashabiki na watu wanaoguswa na ujumbe wa Nay kushiriki kwenye #fundraising kwa lengo
la kumtia moyo Nay ili aendelee na kazi yake ya kuzungumzia matatizo ya kijamii kupitia muziki.

Nay wa Mitego, anayejulikana kwa ujasiri wake wa kuzungumzia masuala nyeti ya kijami, amekuwa akipaza sauti kwa niaba ya raia na kushughulikia changamoto
zinazowakumba wananchi wengi. Katika kipindi ambacho wasanii wengi wamekaa kimya kuhusu masuala haya, Nay ameendelea kuwa kipaza sauti cha haki za wananchi kupitia sanaa yake.

Roma Mkatoliki, akiambatana na mashabiki, walionani muhimu kumtia moyo Nay kwa kumchangia fedha kama ishara ya kumshukuru kwa juhudi zake za kutetea haki za watu.

Michango yote inapelekwa moja kwa moja kwa Nay wa Mitego kupitia akaunti yake ya benki, na simu ikiwa ni ishara ya kumfuta jasho na kumtia mnoyo aendelee
kuzungumza kwa niaba ya wananchi.

Mashabiki na wasanii wameombwa kuendelea kutoa michango yao, licha ya hali ngumu za kiuchumi, ili kuonyesha mshikamano na kuthamini kazi kubwa Nay
anayofanya kwa jami.

Michango hii inaenda mbali zaidi
ya kustream muziki wake au kuhudhuria show zake, kwani inampa msanii huyu nguvu na motisha ya kuendelea na harakati zake za kijami.

Kwa kuchangia kampeni ya #OnyeshaUpendoKwaNayWaMitego, mashabiki wanaonyesha kuwa wanatambua umuhimu wa sanaa kama chombo cha kuleta mabadiliko na haki katika jami.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button