Mke Wa Donald Trump, Melania Trump Apewa Jina La First Lady Asiyeonekana
Mke Wa Donald Trump, Melania Trump Apewa Jina La First Lady Asiyeonekana.

Melania Trump, mke wa mgombea urais wa Republican Donald Trump, amepewa jina la “First Lady asiyeonekana’ kutokana na kutoshiriki sana katika majukumu muhimu ya mke wa rais Marekani.
Tangu alipoingia kwenye jukwaa la siasa mwaka 2016, Melania amekuwa akikiuka mila zilizowekwa na wake wa marais waliopita, akionyesha kuwa sio lazima kufuata kanuni hizo kwa kila hali.
Kwenye kitabu chake kipya cha kumbukumbu, Melania anaweka wazi masuala mbalimbali yaliyomgusa moja kwa moja, kuanzia picha zake za utupu kutoka miaka ya 1990 hadi uvamizi wa FBI kwenye makazi ya Mar-a-Lago mwaka 2022.

Anadai kuwa tukio hilo lilikuwa uingiliwaji wa maisha yake binafsi na kutoa onyo kwa Wamarekani kuhusu jambo hilo.
Melania amekuwa na jicho makini kwenye hatma yake ya kifedha na mtoto wake Barron.
Inasemekana alitumia muda mwingi baada ya mume wake kuwa rais kuboresha mkataba wa ndoa yao.
Pamoja na hayo, Melania amejipatia kipato kupitia mauzo ya NFTs na hotuba kadhaa alizotoa kwenye sherehe za watu maarufu.
Licha ya hivyo, wachambuzi wa historia, kama vile Robert Watson, wanamkOsoa Melania kwa kufanya makosa ya hiari, kama kuvaa koti lenye ujumbe wa “I really don’t care, do u?” alipotembelea watoto waliotenganishwa na wazazi wao mpakani.

Kwa mtazamo wa Watson, mchango wa Melania hauwezi kufikia wake wa marais kama Jackie Kennedy au Michelle Obama.





