Wasanii wa Tanzania Watamba Top 4 Kenya.

Wasanii wa Tanzania Watamba Top 4 Kenya.

Ripoti ya Nairobi Gossip Club imethibitisha kuwa muziki wa Bongo Fleva umeendelea kuwa na ushawishi mkubwa nchini Kenya, huku wasanii wa Tanzania wakiongoza chati za YouTube kwa mwaka mmoja uliopita.

Diamond PlatnumzZ anaongOza kwa watazamaji milioni 127, akifuatiwa na Rayvanny (milioni 81.9), Harmonize (milioni 78.3), na Zuchu, ambaye ni mwanamke pekee kwenye Top 10, akiwa na watazamaji milioni 78.1. Israel Mbonyi kutoka Rwanda amejipatia nafasi ya tano akiwa na watazamaji milioni 74.7.

Chati hii inajumuisha wasanii wengine wa Tanzania kama Mbosso (milioni 54.2), Jay Melody (milioni 52.7), Alikiba (milioni 46.3), na Marioo (milioni 42.3). Kwa upande wa Kenya, Guardian Angel (milioni 61.7), Msanii Music Group (milioni 48.6), na Otile Brown (milioni 41.7) wamewakilishwa kwenye orodha. Ayra Starr kutoka Nigeria na Chris Brown kutoka Marekani pia wameingia kwenye chati hi, wakiwa na watazamaji milioni 43.9 na milioni 47.7.

Kwa ujumla, wasanii 9 kutoka Tanzania wanaongoza chati, huku nyimbo maarufu za Bongo Fleva kama Enjoy ya Jux, Sisi ni Wale ya Phina, na Mapoz ya Diamond Platnumz zikivuma zaidi nchini Kenya.

Orodha ya Chaneli 15 za YouTube zenye watazamaji wengi kwa mwaka mmoja uliopita:

1. @DiamondPlatnumz- milioni 127

 

2. @Rayvanny- milioni 81.9

3. @harmonize_tzZ – milioni 78.3

4. @officialzuchu – milioni 78.1

5. @israelmbonyi – milioni 74.7

6. @guardianangelglobal – milioni 61.7

7. @mbosso_ – milioni 54.2

8. @realjaymelody – milioni 52.7

9. @msanimusicgroup – milioni 48.6

10. @officialalikiba – milioni 46.3

11. @chrisbrownofficial – milioni 47.7

12. @ayrastarr – milioni 43.9

13. @juma_jux – milioni 43.6

14. @marioo_tz – milioni 42.3

15. (@otilebrown – milioni 41.7

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button