Mfanyabiashara wa Madini Auawa Mlima wa Maombi,Wauaji Watuma Meseji.
Mfanyabiashara wa Madini Auawa Mlima wa Maombi,Wauaji Watuma Meseji
Mwili wa mfanyabiashara wa madini
ya ujenzi, David Mollel mkazi wa Kata ya Moivaro, umekutwa ukining’inia kwenye mti juu ya Mlima Oldonyowas, jirani na eneo linalotumika kwa maombi.
Inadaiwa Mollel mwenye umri wa kati ya miaka 50 na 55, aliuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumanne, Oktoba Mosi, 2024 kwa kunyongwa na mkanda wa suruali. Mwili wake ulifunikwa kitambaa chekundu usoni.
Taarifa za awali zinaashiria mgogoro wa kugombea eneo la uchimbaji madini ya ujenzi aina ya moramu ni chanzo cha mauaji hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha tukio hilo akisema uchunguzi umeanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama.