Sababu ya Ongezeko La Mafua na Kifua
Sababu ya Ongezeko La Mafua na Kifua
Wizara ya Afya imesema kuna ongezeko la virusi wanaosababisha homa kali ya mafua
inayoambukiza maarufu influenza, waliyotaja
kusababishwa na mabadilikO ya hali ya hewa.
Homa hiyo ambayo husababisha ugonjwa wa vifua inaongezeka katika baadhi ya maeneo nchini, huku wataalamu wa afya wakitoa angalizo kuacha kutumia
kiholela antibaotiki na badala yake wakiwashauri wagonjwa kuhudhuria vituo vya afya na kunywa maji mengi.
Akizungumza na Mwananchi jana Jumanne, Oktoba 1, 2024, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu amesema magonjwa ya vifua huongezeka na kupungua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Amesema ikiangaliwa mwenendo wa mwaka jana na mwaka huu hakuna tofauti, lakini mara nyingi ni maambukizi ya virusi na wamekuwa wakifuatilia Uviko19 kote nchini kupitia maeneo ya ufuatiliaji zaidi ya 20 nchi
nzima, kupitia sampuli za wagonjwa wanafika vituo vya afya kwa matatizo ya vifua.