Mbowe Akemea Kauli Ya Udini Iliyotolewa Zanzibar.

Mbowe Akemea Kauli Ya Udini Iliyotolewa Zanzibar

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani kauli zilizotolewa zenye viashiria vya udini ambazo zimesikika wakati wazee wa chama hicho walipokuwa wakifanya mkutano na waandishi wa habari Zanzibar.

Mkutano huo ulifanyika Oktoba 01, 2024, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, ambapo mmoja wa wazee hao alisikika akiitaka Serikali kufanya maamuzi ya kujiunga na Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (01C) pindi ambapo viongozi wengi ni wa dini ya Kiislamu.

“Tunajitenga na kauli zote zilizotolewa zenye viashiria vya udini kwani huo sio msimamo wa chama na zinapaswa kupingwa na kila Mtanzania bila kujali dini, kabila au mahali alipotoka’ imeeleza taarifa iliyotolewa na CHADEMA kwa vyombo vya Habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button