“Me Too”Ndio Collaboration Kubwa Tangu Mwaka Uanze.
"Me Too" Ndio Collaboration Kubwa Toka Mwaka Uanze.
Wimbo “Me Too” wa Abigail Chams umetimiza mwezi mmoja tangu kuachiwa Februari 28, 2025, na umeendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki.
Mwanzo ulionekana kupokewa kwa Utulivu, lakini sasa umechukua nafasi kubwa kwenye mitaa, huku ukibakia kuwa miongoni mwa nyimbo zinazopendwa zaidi Afrika Mashariki.
Katika kipindi cha mwezi mmoja, wimbo huu umechukua nafasi ya kwanza kwa nyakati tofauti hapa Tanzania, ukithibitisha umaarufu wake mkubwa. Mpaka sasa, video ya “MeToo” imetazamwa mara milioni 4.5 kwenye YouTube, ikiwa video ya pili ya Abigail, yenye watazamaji wengi baada ya “Nani” aliyoshirikiana na Marioo, ambayo ina watazamaji milioni 11 ndani ya miaka miwili.
Kwenye jukwaa la AppleMusic, “Me Too” unashika nafasi ya kwanza Tanzania, nafasi ya pili Uganda, na nafasi ya nane Kenya, jambo linaloonyesha kuwa muziki wa Abigail unazidi kusambaa kimataifa.
Kwa mujibu wa maoni ya mashabiki, sauti ya Abigail kwenye wimbo huu imebeba utulivu mkubwa, huku Harmonize akiongeza ustadi wake wa muziki kama mwanaume mwenye mapenzi mengi.
Video yake haina mambo mengi, inawaonyesha wao wawili kama wahusika wakuu, jambo ambalo limeongeza upekee wa kazi hii. Abigail na Harmonize wameshirikiana kwenye nyimbo tatu tofauti, lakini “Me Too” imeonekana kupendwa zaidi kuliko “Closer” na “Leave Me Alone”.
Wimbo huu umeweza kuunganisha mashabiki wa aina mbalimbali na kuwafanya waone upekee wa Abigail kama msanii anayeibukia kwa kasi kwenye soko la kimataifa.
Abigail kwa mafanikio haya, ni vyema pia kumpongeza Harmonize kwa mchango wake mkubwa katika wimbo huu.
Uwepo wake umeongeza mvuto wa “Me Too”, na kwa pamoja wameweza kupeleka Bongo Fleva kwenye viwango vya kimataifa.
Mashabiki wengi sasa wanamfananisha AbigailChams na VanessaMdee, wakiamini kuwa anaelekea kuwa msanii wa hadhi ya kimataifa kama Vee Money lkiwa ukuaji wa wimbo huo utaendelea na mwelekeo huu, huenda ukawa ni kolabo kubwa zaidi ya Bongo Fleva mwaka huu, kulingana na umaarufu wake, kulinganisha na nyimbo nyingine za kushirikiana.