Muigizaji Wa Batman Forever Afariki Dunia.

Muigizaji Wa Batman Forever Afariki Dunia.

Mwigizaji Val Kilmer aliyewahi kuvaa vazi la Batman katika filamu ya Batman Forever (1995) amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65 kutokana na nimonia, Kilmer ambaye pia alijulikana kwa majukumu yake katika filamu kama Top Gun na The Doors aligunduliwa kuwa na saratani ya koo mwaka 201 4 hali iliyomsababisha kupoteza uwezo wake wa kuzungumza kikamilifu.

Kilmer alizaliwa Desemba 31, 1959 mjini Los Angeles na alikuwa mmoja wa Wanafunzi wachanga zaidi kupokelewa katika programu ya uigizaji ya Juilliard akiwa na umri wa miaka 17 ambapo alianza kupata umaarufu kupitia filamu ya Top Secret! (1984) kabla ya kuigiza kama lceman katika Top Gun (1986) kisha kuchukua nafasi ya Jim Morrison katika The Doors (1991)

Ingawa alihusika katika filamu kubwa kama Batman Forever Kilmer alikumbwa na changamoto za kiafya katika miaka yake ya mwisho na Saratani ya koo aliyopata ilisababisha apitie matibabu makali yakiwemo upasuaji wa sehemu ya koo lake ambao uliathiri sauti yake

Katika miaka ya baadaye Kilmer aliendelea kushiriki katika miradi midogo ya uigizaji, Kilmer ameacha Watoto wawili Mercedes na Jack ambao alizaa na Mke wake wa zamani mwigizaji Joanne Whalley.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button