Wizara Yatoa Ufafanuzi Mzazi Anayedai Kubadilishiwa Mtoto.

Wizara Yatoa Ufafanuzi Mzazi Anayedai Kubadilishiwa Mtoto

Wizara ya Afya imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Bi. Neema Kilugala, mkazi wa Daraja Mbili, Arusha, anayelalamikia kubadilishiwa mtoto wake baada ya
kujifungua kwa njía ya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, tarehe 24 Machi 2025.

Kwa mujibu wa Bi. Neema, baada ya kujifungua alionyeshwa mtoto wake akiwa mzima, lakini baadaye aliletewa mtoto akiwa amefungwa na vitenge ambavyo si vyake.

Muuguzi aliyekuwa akimhudumia alidai kuwa
kulikuwa na kuchanganywa kwa vitenge na vya mtoto mwingine na kuahidi kurekebisha hali hiyo, lakini hali ya sintofahamu iliendelea
Kutokana na tukio hilo,

Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha pamoja na Jeshi la Polisi, imechukua hatua zifuatazo:

1. Kuchukua sampuli za wazazi waliojifungua katika kipindi hicho pamoja na watoto kwa uchunguzi wa vinasaba (DNA) katika Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali

2. Kumsimamisha kazi muuguzi aliyemhudumia Bi. Neema ili kupisha uchunguzi.

Wizara ya Afya imesema kuwa taarifa rasmi zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika na hatua stahiki zitachukuliwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button