Mfanyakazi mochwari asimamishwa kwa tuhuma kulazimisha wafiwa kununua majeneza yake

Mfanyakazi mochwari asimamishwa kwa tuhuma kulazimisha wafiwa kununua majeneza yake

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure imemsimamisha kazi mtumishi wake katika Kitengo cha Mochwari baada ya kudaiwa kulazimisha wafiwa kununua majeneza kwake.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa hospitali hiyo, Elidaima Kimaro leo Jumatano Aprili 22, 2026 imesema mtumishi huyo alikuwa anauza majeneza hivyo kuwalazimisha wafiwa kununua kwake.

“Tumepokea taarifa ya mtumishi Kitengo cha Mochwari anayeuza majeneza na kulazimisha wafiwa kununua kwake na tayari umeshachukua hatua za haraka za kumsimamisha kazi mtumishi huyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo,” imesema taarifa hiyo.

Hospitali hiyo imewataka wananchi wanaokutana na changamoto ya aina hiyo kuwasiliana na hospitali kupitia namba za simu za viongozi zilizobandikwa kwenye mbao za matangazo hospitalini hapo.

Pia, wametakiwa kutoa taarifa kupitia masanduku ya maoni yaliyowekwa katika kila idara kwa ajili ya kupokea maoni, mapendekezo na changamoto yoyote kutoka kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button