Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshiriki katika hafla ya kupokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Kodi,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshiriki katika hafla ya kupokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Kodi, iliyofanyika leo tarehe 18 Machi 2026, Ikulu, Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipokea ripoti hiyo kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Mhe. Balozi Ombeni Yohana Sefue ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi nchini.
Tume hiyo iliundwa kwa lengo la kufanya tathmini ya mifumo ya kodi, mapato na tozo mbalimbali nchini, kwa kukusanya maoni ya wadau ili kubaini changamoto zilizopo na kupendekeza maboresho yatakayosaidia kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kupunguza kero kwa walipa kodi pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.






