MHE.NDEJEMBI AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI NYARAKA ZA KIBAJETI WIZARA YA NISHATI 2026/2027

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo ameongoza kikao cha kupitia nyaraka mbalimbali za Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2026/2027 kabla ya kuiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ( Petroli na Gesi Asilia), Dkt.James Mataragio, Menejimenti ya Wizara ya Nishati pamoja na wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Kikao hicho pia kimejadili utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Mwaka 2025/2026 pamoja na randama ya Bajeti ya Wizara ya mwaka 2026/2027.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button