Mhe. Dkt. Mwigulu, amesema wamelipa Deni shilingi trilioni 8.48
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Bungeni Jijini Dodoma amewasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya makadairio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/2025, amesema mwaka wa fedha 2023/2024 Bunge la Tanzania liliidhinisha jumla ya shilingi trilioni 10.48 kwa ajili ya kuhudumia deni la Serikali pindi linapoiva.
Mhe. Dkt. Mwigulu, amesema hadi Aprili 2024 wizara imelipa kwa wakati notisi za madai ya deni lililoiva jumla ya shilingi trilioni 8.48, sawa na ufanisi wa asilimia 81 ya lengo la mwaka, kati ya kiasi hicho, deni la ndani ni shilingi trilioni 4.63, ikijumuisha riba shilingi trilioni 1.98 na mtaji shilingi trilioni 2.65, na deni la nje ni shilingi trilioni 3.83, ikijumuisha riba shilingi trilioni 1.34 na mtaji shilingi trilioni 2.49.






