Mhe. Jumaa Aweso (Mb), akimkaribisha Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Elke Wisch,

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), akimkaribisha Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Elke Wisch, pamoja na ujumbe wake katika ofisi za Wizara ya Maji, Mtumba jijini Dodoma, kabla ya kuanza kikao cha kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya maji, usafi wa mazingira na afya (WASH).

Mhe. Aweso amejumuika na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, Naibu Katibu Mkuu, Bi. Rose Ambrose, pamoja na wakurugenzi wa Wizara ya Maji.

Kikao hicho kililenga kutathmini mafanikio ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali na UNICEF na kujadili maeneo mapya ya ubia yatakayochangia kuimarisha huduma za maji safi na salama, usafi wa mazingira na afya kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button