Trending

Miaka Mitatu Imetimia Tangu Hayati Benjamin Mkapa Afariki Dunia.

  1. Leo Jumatatu, Julai 24, 2023 ni miaka mitatu imetimia tangu Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa alipofariki dunia katika Hospitali jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mkapa alifariki dunia Julai 24, 2020 akiwa na miaka 81. Alizaliwa Novemba 12, 1938, Lupaso, Masasi mkoani Mtwara. Ndipo
alipozikwa Julai 29, 2020.

Aliiongoza Tanzania kwa nafasi ya urais kwa miaka kumi mfululizo kuanzia 1995-2005.

Mkapa alifariki dunia mwaka mmoja tangu alipozindua kitabu cha maisha binafsi ya Rais mstaafu wa Tanzania, kinachoitwa ‘My life, My purpose’ (Maisha Yangu, Kusudio Langu).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button