Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume amesema kila mtu anapaswa kufahamu umoja wetu unatokana na Muungano

Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume amesema kila mtu anapaswa kufahamu umoja wetu unatokana na Muungano,hali hiyo inasababisha kila mmoja anamthamini mwenzake na kumwona ndugu yake. Umoja na udugu huu ni kutokana na misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili.

Amesema Hayati Mzee Karume na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyeyere waliona vyema mataifa haya kuungana kutokana na ukaribu wa wananchi wa mataifa haya (Tanganyinga na Zanzibar).

Mama Fatma Karume ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Massauni mara alipomtembelea nyumbani kwake Zanzibar, Disemba 11, 2025 huku akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Ofisi ya Makamu wa Rais

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button