Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kumuombea Marehemu Jenista Mhagama
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kumuombea Marehemu Jenista Mhagama leo Desemba 13, 2025 inayofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma.
Marehemu alikuwa Mbunge wa Peramiho tangu mwaka 2005 na amefariki Dunia Siku ya Alhamisi, Desemba 11, 2025 Jijini Dodoma, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa Desemba 14, 2025 kuelekea Mkoa wa Ruvuma ambako mazishi yatafanyika siku ya Jumanne Disemba 16, 2025 katika kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga.






