Mtindo wa Majeneza Ghana Unashangaza Dunia.

Mtindo wa Majeneza Ghana Unashangaza Dunia

Nchini Ghana, hususan kwa jamii ya Waga (Ga) wanaoishi maeneo ya pwani karibu na Accra, kifo hakihesabiwi kama mwisho wa maisha bali kama sherehe ya safari mpya. Hapo ndipo hutokea “Fantasy Coffins” jeneza za kipekee zinazotengenezwa kwa maumbo ya vitu vinavyohusiana moja kwa moja na maisha au ndoto za marehemu.

Badala ya jeneza la kawaida, unaweza kukutana na jeneza lililochongwa kama ndege, samaki, gari, kiatu, simu au hata rundo la pesa. Kila umbo huashiria heshima na hadithi ya yule aliyefariki.

Asili yake inahusishwa na fundi maarufu Seth Kane Kwei miaka ya 1950, aliyeanzisha mtindo huu baada ya kutengeneza jeneza la umbo la ndege kumuenzi bibi yake aliyetamani kusafiri angani. Tangu hapo, warithi wake kama Paa Joe na mafundi wengine wameendeleza sanaa hii, na leo jeneza hizi zimekuwa sehemu ya makumbusho na maonyesho duniani.

Zaidi ya kuwa sehemu ya mazishi, fantasy coffins zimekuwa kielelezo cha maisha, utu na heshima, zikionesha kuwa hata safari ya mwisho inaweza kujaa rangi, ubunifu na furaha ya kukumbuka maisha ya mtu.

Kama ungetengeneza fantasycoffin yako, ingekuwa na umbo gani?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button