Wimbo wa Diamond na Ciara “LOW” imeandikwa na Watu Wanne

Wimbo wa Diamond na Ciara "LOW" imeandikwa na Watu Wanne

Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu kuandikiwa nyimbo. Wapo wanaoona ni udhaifu, na wapo wanaoona ni sehemu ya kazi. Lakini kinachoonekana wazi ni kwamba uandishi wa nyimbo ni biashara rasmi, kuna watu kazi yao kubwa ni kuandika mashairi, bila hata wao kuimba, na hulipwa vizuri kwa kipaji hicho.

Wimbo mpya wa Ciara – Low ft. Diamond Platnumz ni mfano halisi wa namna biashara inavyofanyika kitaalam. Wimbo huo wa dakika 3:30, umeandikwa na watu wanane, wakiwemo Ciara na Diamond wenyewe. Diamond Platnumz, ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul Juma Isaack, amepewa credit kama mwandishi, jambo linalothibitisha kwamba hakusimama tu kama msanii aliyealikwa, bali pia alihusisha mawazo yake binafsi kwenye wimbo huu.

Waandishi wa “Low”:

Ciara

Naseeb Abdul Juma Isaack (Diamond Platnumz)

Charlotte Wilson

Courtlin Jabrae

Darius Logan

Dominique Logan

Magnus Klausen

Ebenezer Fabiyi (ambaye pia ni mtayarishaji wa wimbo huo).

Hii ni hatua kubwa kwa Diamond Platnumz kwa sababu ameweka jina lake kama mwandishi kwenye albamu ya kimataifa ambayo pia inawakutanisha mastaa wakubwa kama Chris Brown, Busta Rhymes, Tyga, Lil Baby na wakali wengine. Kila shairi aliloandika Diamond limeongeza thamani na ladha muhimu ya Bongo Fleva ndani ya albamu hiyo ya ‘CiCi Deluxe’.

Kwa hiyo, dhana kwamba kuandikiwa nyimbo ni udhaifu haina mashiko. Badala yake, inapaswa kuonekana kama kazi ya ubunifu wa pamoja, kila mwandishi akileta kipande chake cha ubunifu ili kuunda wimbo bora zaidi. “Low” ni ushahidi kwamba muziki mzuri ni matokeo ya nguvu za wengi, na heshima ya Diamond kwenye kazi hii ni ya kihistoria kwa muziki wa Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button