Mtoto wa Miaka 10 Mbaroni kwa Tuhuza za Wizi wa Gari

Mtoto wa Miaka 10 Mbaroni kwa Tuhuma za Wizi wa Gari

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro
linachunguza tukio la mtoto mwenye miaka 10 mwanafunzi wa darasa la tano, ambaye anandaiwa kukamatwa kwa tuhuma za wizi wa gari aina ya Spacio mali ya Zuhura Khatibu (47), mkazi wa Kilakala Manispaa
ya Morogoro

Mtoto huyo amekamatwa jana Mei 26, 2025, asubuhi katika eneo la Kigurunyembe akiwa anaendesha gari hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Alex Mkama amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtoto huyo, akiwa na
wenzake ambao bado wanatafutwa, walitumia funguo bandia kuendesha gari hilo

Aidha Kamanda Mkama amesema taarifa kamili itatolewa baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika, Baadhi ya mashuhuda akiwemo Paul Boniface amesema mtoto huyo amekamatwa baada ya kugongana na
bodaboda katika eneo la Kigurunyembe akiendesha gari hilo, baada ya kugongana alikimbia wananchi wakamkimbiza na kumkamata akiwa amejificha kwenye
shimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button