MWIGULUNCHEMBA NA ANGELLA KAIRUKI MAWAZIRI KATIKA PICHA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba , akiwa katika picha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhe. @angellah_kairuki , baada ya Mhe. Dkt. Nchemba, kuwasilisha mada ya hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2023/2024, katika mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa iliyoandaliwa na TAMISEMI katika Shule ya Uongozi ya Julius Nyerere-Kibaha mkoani Pwani, na kuwataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kusimamia ipasavyo makusanyo ya mapato ya ndani pamoja na kulinda biashara ili kuiwezesha Serikali kupata mapato yatakayofanikisha kutekeleza miradi yake inayolenga kuchochea maendeleo ya nchi pamoja na kuimarisha sekta za uzalishaji na kukuza ajira