Ophrah Avuna Mamilioni Kampeni za Kamala.

Ophrah Avuna Mamilioni Kampeni za Kamala.

Kampeni ya Makamu wa Rais Kamala Harris ilitumia zaidi ya dola milioni 1 kuilipa kampuni ya Harpo Productions inayomilikiwa na Oprah Winfrey, kwajili ya shughuli mbalimbali za uchaguzi.

Mwezi Septemba, Winfrey alishiriki kwenye ukumbi wa mjadala na Harris, kisha alihudhuria mkutano wa mwisho wa Harris mjini Philadelphia siku moja kabla ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa ripoti ya “Washington Examine’*, kampeni hiyo pia ilitumia kiasi kikubwa kuandaa sehemu ya kurekodi kwa mahojiano ya Harris kwenye podcast maarufu ya ‘Call Her Daddy’ yenye mtangazaji Alex Cooper.

Mahojiano haya yalirekodiwa katika hoteli moja mjini Washington, D.C., na kutolewa Oktoba.

Aidha, kampeni ya Harris iliandaa matamasha katika majimbo muhimu ya ushindani siku chache kabla ya uchaguzi.

Matamasha hayo yalijumuisha wasanii kama Jon Bon Jovi, Christina Aguilera, Katy Perry, Lady Gaga, na 2 Chainz, ambao walipanda jukwaani kusaidia kampeni.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa kama Brad Todd maamini kuwa matumizi haya hayakutosha kubadili mwelekeo wa wapiga kura, huku wakidai kampeni ya Harris ilikosa ujumbe unaovutia na kujitenga na utawala uliokuwa na umaarufu mdogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button