MTV EMA: Ushindi wa Tyla Wawagawa Wafrika.
MTV EMA: Ushindi wa Tyla Wawagawa Wafrika.
Ushindi wa msanii kutoka Afrika Kusini, Tyla, katika kipengele cha “Best Afrobeat” kwenye tuzo za MTV EMA umewasha moto mtandaoni, huku mashabiki wengi wakishangaa jinsi msanii ambaye hajawahi kuimba muziki wa Afrobeat alivyoweza kushinda tuzo hiyo.
Mashabiki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, hasa Nigeria, wamejitokeza wakipinga ushindi huo kwa madai kuwa Tyla haufanyi muziki wa Afrobeat bali anajulikana zaidi kwa Amapiano na Pop.
Wengine walilalamika kwamba waandaaji wa tuzo hizo hawajali utofauti wa muziki wa Kiafrika, huku kila aina ya muziki wa Afrika ikikabidhiwa jina la Afrobeat.
Kuna wengine walionekana kumtetea Tyla, wakisema kuwa ushindi ni ushindi na kwamba hakika Tyla ni msanii mwenye kipaji na anayepaswa kusifiwa kwa hatua aliyofikia.
Pamoja na hayo, mjadala huu unaonyesha jinsi Afrobeat imekuwa sehemu ya utambulisho wa kitamaduni na muziki wa Kiafrika, na namna mashabiki wanavyoilinda aina hiyo ya muziki, wakiwa hawataki ichanganywe na mambo mengine yasiyohusiana.