Papa Atembelea Msikiti Mkuu Algiers
Papa Atembelea Msikiti Mkuu Algiers
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, ametembelea Msikiti Mkuu wa Algiers April 13, 2026, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 11 Barani Afrika.
Akiwa ndani ya Msikiti huo maarufu unaojulikana pia kama “Msikiti wa Algeria”, Papa Leo XIV alivua viatu vyake kabla ya kuingia, ishara ya heshima inayozingatiwa katika maeneo ya Ibada ya Kiislamu, ziara hiyo imebeba uzito mkubwa wa kidini na kijamii, ikionyesha jitihada za kuimarisha uhusiano kati ya Waumini wa Dini tofauti pamoja na kukuza amani na mshikamano duniani
Hatua ya Papa kutembelea Msikiti huo inaendelea kuonyesha msimamo wa kuheshimu tamaduni na imani za Watu mbalimbali katika jamii za kimataifa, hii inaongeza kwenye rekodi yake ya ziara za maeneo ya Ibada ya Kiislamu, ambapo awali aliwahi kutembelea Msikiti wa Blue Mosque, akiendeleza ujumbe wa kuheshimiana kati ya Dini.






