SERIKALI YASAINI MIKATABA YA UNUNUZI NA USAFISHAJI DHAHABU

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Benki Kuu ya Tanzania imesaini mikataba ya ununuzi na usafishaji dhahabu na kampuni za uchimbaji madini na Kiwanda cha Usafishaji Dhahabu cha Geita Gold Refinery (GGR), hatua itayowezesha Benki Kuu kupata vyanzo vya uhakika katika kufanikisha programu yake ya ununuzi wa dhahabu.

Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square jijini Dodoma kati ya Gavana wa Benki Kuu na Kampuni za madini wakishuhudiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Dkt.Nchemba alisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini ambacho kinawataka wachimbaji wa madini kutenga asilimia 20 ya uzalishaji wao kwa ajili ya kuiuza katika masoko ya ndani ikiwemo kuiuzia Benki Kuu ya Tanzania, ambayo imepewa haki ya kwanza kisheria ya ununuzi wa dhahabu.

‘‘Sambamba na hiyo, hatua hii itaiwezesha Benki Kuu kupata vyanzo vya uhakika katika kufanikisha programu yake ya ununuzi wa dhahabu na itasaidia viwanda vya ndani vya usafishaji wa dhahabu kufikia malengo ya kupata ithibati ya kimataifa ya London Bullion Market Association (LBMA)’’, alifafanua Dkt. Nchemba.

Alisema kuwa mpango wa ununuzi wa dhahabu ni dhamira ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, kuongeza mchango wa madini katika pato la Taifa, pamoja na kuongeza thamani ya madini nchini ili kuhakikisha wananchi wote wananufaika na rasilimali za madini.

‘‘Hadi leo Benki Kuu ya Tanzania, imenunua tani 5 za dhahabu sawa na dola za Marekani milioni 554 na kupitiliza malengo yake ya kununua dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani milioni 350, Hatua hii ni kubwa na ya kihistoria nchini kwetu, kwa kuwa itatuhakikishia kuwa na dhahabu ya kutosha hapa nchini kwa ajili ya kusafishwa na viwanda vilivyopo hapa nchini, lakini pia kuipa Benki Kuu ya Tanzania, ambayo imeamua kununua na kutunza dhahabu kama sehemu ya fedha za kigeni’’, alifafanua Mhe. Dk

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button