Trump Atangaza Kiama Hamasi Wasipoachia Mateka Wa Israel

Trump Atangaza Kiama Hamasi Wasipoachia Mateka Wote wa Israel

Rais wa Marekani, Donald Trum ametangaza kile alichokita onyo la mwisho kwa wapiganaji wa kundi la Hamas akiwataka kuwaachia mateka wote walioko eneo la Gaza, huku akitangaza kiama endapo hawatofanya hivyo.

CNN imeripoti leo Alhamisi Machi 6, 2025, kuwa Trump ametangaza uamuzi huo baada ya Marekani kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kundi la Hamas.

“Waachilieni mateka wote sasa hivi na siyo baadaye na mrejeshe mara moja mili ya watu mliowaua la sivyo “mtakuwa mmekwisha.”

Trump aliandika kwenye akaunt yake ya Truth Social, muda mfupi baada ya kukutana na mateka wanane waliokuwa wameachiwa kutoka Gaza.

Trump aliandika kuwa ataitumia Israel kila kitu inachohitaji kukamilisha kazi na akaonya kuwa: “Hakuna hata mshirika mmoja wa Hamas atakayekuwa salama msipofanya ninavyosema.”

Matamshi hayo yalitolewa saa chache tu baada ya Marekani kuthibitisha ripoti kwamba ilikuwa inafanya mazungumzo ya moja kwa moja na Hamas kuhusu mateka na usitishaji mapigano Gaza, hatua ambayo ni kinyume na sera yake ya kawaida ya kutofanya mazungumzo na makundi inayoyachukulia kuwa ya kigaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button