Bodi Ya Ligi: Mechi Ya Yanga na Simba Iko Palepale Njooni Kwa Mkapa

Bodi Ya Ligi: Mechi Ya Yanga na Simba Iko Palepale Njooni Kwa Mkapa

Sakata la Simba kugomea mchezo dhidi ya watani wao, Yanga, limechukua sura mpya baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutoa tamko kwamba mechi hiyo ipo palepale kama ilivyopangwa.

Simba ilitoa tamko usiku wa kuamnkia leo ikisema haitaleta timu uwanjani kwenye mchezo huo kufuatia msafara wa kikosi chake kuzuiwa jana usiku kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambao ndio utatumika kwenye mechi hiyo.

Simba ilizuiwa na kundi la watu wanaodhaniwa ni mashabiki wa Yanga maarufu kwa jina la makomando, huku pia ikimtaja meneja wa uwanja kudai hakuwa na taarifa kwamba Wekundu hao watakwenda kufanya mazoezi uwanjani hapo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Steven Mnguto amesema licha ya Simba kudai haitaleta timu mchezo huo upo palepale huku akiwataka mashabiki waliokata tiketi kujipanga kwenda uwanjani.

“Matukio yote tumeyasikia na tunayafuatilia kuanzia hatua ambayo yalijiri, kuna ripoti za awali tumeshazipokea kwa wasimamizi mbalimbali na tunazifanyia kazi,”‘ amesema Mnguto.

“Kwanza niwatoe wasiwasi mashabiki wa soka na wadau kwa ujumla. Mchezo upo palepale kama ambavyo kalenda yetu ya soka inavyosema, hakuna mabadiliko yoyote, mashabiki wajipange kuja kutazama mchezo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button