Tyler Perry Ashtakiwa Tuhuma za Unyanyasaji Wakingono.
Tyler Perry Ashtakiwa Tuhuma za Unyanyasaji Wakingono.
Unaambiwa Timu Ya Wanasheria Wa Muigizaji Maarufu Wa Marekani, @tylerperry Imeibuka Na Kukanusha Madai Yanayomkabili Perry, Baada Ya Mmoja Kati Ya Waigizaji Wa Filamu Yake Ya #TheOval ‘Derek Dixon’ kumfungulia kesi ya unyanyasaji wa kingono. Kwa mujibu wa @TMZ_tv, Derek anadai fidia ya dola milioni 260 (Tsh Bilioni 680/=).
Derek anadai alikutana na Perry kwenye hafla moja 2019, ambapo Perry alimuita kutoka kwenye kundi la watu na kumuomba namba ya simu akiahidi huenda angempa nafasi ya kuigiza. Baadaye, Derek alipata nafasi Ya Kuigiza katika episode 2 Za Filamu Ya Perry litwayo “Ruthless.”
Kwa mara nyingine tena, Januari 2020, Derek Alialikwa Nyumbani Kwa Perry jijini Atlanta, Ambapo Anadai Usiku Alilewa Sana Na Kisha Kulazwa Chumba cha Wageni. Akiwa Amelala anadai Perry aliingia chumbani na kuanza kumshika mapajani. Derek anasema alikataa vitendo hivyo. Baadaye, alipewa nafasi ya kuigiza kama Dale katika Filamu Ya “The Oval”, lakini pia anadai Perry alianza kumtumia Text Zenye Maudhui Ya Kingono.
“Perry Hawezi Kuyumbishwa, Mipango Ya Kumuangusha Perry Itagonga Mwamba” – Amesema Mwanasheria Wake Mathew Boyd