Uingereza Kugawa Umeme Bure kwa Wananchi

Uingereza Kugawa Umeme Bure kwa Wananchi

Serikali ya Uingereza imesema kuwa imefanya maboresho katika sekta ya umeme, hatua inayotarajiwa kuwanufaisha Wananchi kwa kuwapatia umeme wa bure au wa gharama nafuu endapo watatumia vifaa vyao vya umeme wakati wa siku za jua kali, hasa mwishoni mwa wiki.

Maboresho hayo yanatekelezwa kupitia mpango unaosimamiwa na Mfumo wa Nishati wa Kitaifa (NESO), ambao umeboreshwa ili kukabiliana na ongezeko la uzalishaji wa nishati mbadala kama sola, lengo kuu ni kuhakikisha umeme unaozalishwa kwa wingi haupotei bali unatumiwa kwa ufanisi.

Hatua hiyo imeidhinishwa na mdhibiti wa sekta ya nishati Ofgem, ambaye ameruhusu mabadiliko ya mfumo uliokuwa ukilenga kupunguza matumizi saa ambazo watu wanatumia huduma hiyo zaidi na pia kuhamasisha matumizi zaidi pale uzalishaji unapozidi mahitaji.

Kupitia maboresho hayo, Wananchi watahamasishwa kutumia umeme huo kwa kuendesha vifaa kama mashine za kufulia, dishwashers na kuchaji magari ya umeme katika nyakati hizo.

Maboresho hayo yanaonekana kuwa hatua muhimu katika kupunguza upotevu wa nishati mbadala, kuongeza ufanisi wa mfumo wa umeme na kupunguza utegemezi wa nishati ya mafuta, huku yakitoa nafuu kwa wananchi katika gharama za maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button