Vita Vinanyong’onyeza Moyo Wangu

Vita Vinanyong'onyeza Moyo Wangu

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, amekemea vikali vita na migogoro mbalimbali duniani, akisema hali hiyo imeunyong’onyeza moyo wa Mungu kutokana na mateso, ukosefu wa haki na kuenea kwa vurugu katika jamii.

Akiwa katika ziara Nchini Algeria, Papa ametembelea Mji wa Annaba, alikozaliwa Mtakatifu Augustine, na kueleza kuwa mafundisho ya Mwanatheolojia huyo ndiyo yaliyomvutia kujiunga na Upadri na kuendelea kuwa mwongozo muhimu katika imani ya Kikristo.

Aidha, katika mazungumzo yake na Watawa na Wazee wachache, Papa Leo XIV amesema moyo wa Mungu unahuzunishwa na vita, ukosefu wa haki, uwongo na machafuko yanayoendelea duniani, akisisitiza umuhimu wa kurejesha maadili na mshikamano wa kibinadamu, ziara hiyo, ni ya kwanza kwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Nchini Algeria, ikiwa imelenga kuhimiza amani na mshikamano kati ya Wakristo na Waislamu, licha ya kuripotiwa kwa mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga hivi karibuni katika Mji wa Blida karibu na Algiers.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button