Malema Ahukumiwa Miaka 5 Gerezani

Malema Ahukumiwa Miaka 5 Gerezani

Kiongozi maarufu wa upinzani Nchini Afrika Kusini, Julius Malema, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano Jela baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki silaha kinyume cha sheria na kupiga risasi hadharani.

Katika tukio lililotokea mwaka 2018, video ilionyesha Malema akitumia bunduki ya kijeshi (semi-automatic) kupiga risasi kadhaa angani wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka mitano ya Chama chake, Economic Freedom Fighters (EFF), huko katika mkoa wa Eastern Cape.

Katika utetezi wake, Malema alidai kuwa silaha hiyo haikuwa yake na kwamba alifyatua risasi hizo ili kuvutia umati wa Watu, kama ilivyoripotiwa na tovuti za habari wakati huo.

Hukumu hii ya leo April 16, inakuja wakati ambapo hali ya kisiasa nchini Afrika Kusini ni tete, ambapo Malema ameendelea kuwa kiongozi mwenye sauti kubwa katika Siasa za upinzani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button